Hamia kwenye habari

Hamia kwenye menyu ya pili

Mashahidi wa Yehova

Kiswahili

FEBRUARI 14, 2013
URUSI

Urusi: Yazuia Uhuru wa Kukusanyika Kinyume cha Sheria

Urusi: Yazuia Uhuru wa Kukusanyika Kinyume cha Sheria

Mnamo Desemba 5, 2012 Mahakama ya Katiba nchini Urusi iliidhinisha kwamba si lazima mashirika ya kidini yapate kibali cha serikali muda fulani mapema kabla ya kufanya mikutano ya kidini nje ya mahali pao pa ibada panapotambuliwa rasmi. Kesi hiyo, iliyoanzishwa na Mchunguzi Maalumu wa Haki za Binadamu wa serikali ya Urusi anayeshughulikia malalamiko ya wananchi, ilikuwa muhimu sana kwa Mashahidi wa Yehova ambao hupanga makusanyiko ya kila mwaka na kuyafanya katika mahali pa kukodishwa na katika nyumba binafsi. Katika kufikia uamuzi wake, Mahakama hiyo ya Katiba ilitegemea ushindi mbalimbali ambao Mashahidi wa Yehova walipata katika Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu. Grigory Martynov, msemaji wa Mashahidi wa Yehova, alisema hivi: “Tunatumaini kuwa uamuzi huo utaturuhusu kukutanika bila kizuizi chochote na kwamba unaunga mkono uhuru wa kuabudu nchini Urusi.”

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

J. R. Brown, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1 718 560 5000

Urusi: Grigory Martynov, simu +7 812 702 2691