Mahojiano na Daktari Pia Di Benedetto.
“Kwa kufanya mipango mizuri na mikakati yenye malengo, inawezekana kufanya upasuaji hata mkubwa bila kutumia damu.”
Mahojiano na Daktari Pia Di Benedetto.
“Kwa kufanya mipango mizuri na mikakati yenye malengo, inawezekana kufanya upasuaji hata mkubwa bila kutumia damu.”
Mahojiano na Daktari Patrizio Mazza.
“Ni jambo linalowezekana kabisa kutibu uvimbe kama vile lymphoma (aina fulani ya kansa), iwe inaanza au hata aina nyingine za kansa ya damu, pamoja na myeloma (ugonjwa ambao unaongezeka kwa kasi katika nchi za Magharibi) bila kutia damu mishipani.”
Mahojiano na Daktari Alfredo Guglielmi.
“Mashahidi wa Yehova wametusaidia kuwa waangalifu sana tunapotumia damu kwa kumtayarisha mgonjwa vizuri, kumjua mgonjwa vizuri, kwa kupanga njia zinazofaa kutumika ili kutotumia damu nyingi katika chumba cha upasuaji na kwa kutumia njia za kuepuka upungufu wa damu kabla ya upasuaji.”
Kesi ya Mahakama Makuu Inapokaribia, Aliyekataa Kujiunga na Jeshi Apata Tumaini
Agosti 30, 2018, Mahakama Kuu ya Korea Kusini itasikiliza kesi mbele ya umma ili kuchunguza maagizo yaliyotolewa na Mahakama ya Kikatiba ya kutoa utumishi wa badala wa kiraia kwa ajili ya watu wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.
Urusi Yataifisha Ofisi ya Tawi
Kabla ya kusikilizwa kwa rufaa hiyo, mwandishi wa habari, mtaalamu wa kidini, na mawakili wawili Mashahidi walifunua kwamba huo ni ukosefu wa haki wa nchi ya Urusi kutaifisha iliyokuwa ofisi ya tawi.
Chuo Kikuu cha Padua Kimefanya Kongamano la Kihistoria la Kuzungumzia Maendeleo ya Matibabu Yasiyohusisha Damu
Kwa muda fulani, ilionekana kwamba kumtia mgonjwa damu mishipani hakuna madhara yoyote na ndiyo mbinu inayoweza kuokoa uhai wakati wa matatizo makubwa ya kiafya au wakati wa upasuaji tata. Lakini wasemaji wengi katika kongamano hilo walipinga wazo hilo.
Mahojiano na Profesa Antonio D. Pinna.
“Kwa kweli, sidhani daktari anapaswa kumtendea mgonjwa kwa njia tofauti kwa msingi wa dini. Kwa mfano, kuna wagonjwa ambao si Mashahidi wa Yehova na bado hawataki kutiwa damu mishipani.”
Mahojiano na Daktari Luca P. Weltert.
“Watu hawatiwi damu sana mishipani, na si wagonjwa Mashahidi tu, bali wagonjwa ulimwenguni pote, kwa sababu uthibitisho unaonyesha kwamba kutotia damu kunakuwa na matokeo mazuri zaidi.”
Mahojiano na Profesa Massimo P. Franchi
“Ninathamini kwamba nimekutana na Mashahidi wa Yehova katika taaluma yangu. Wamenifanya mimi nikiwa daktari anayetumia mbinu za kawaida za tiba, kuanza kuchunguza uwezekano na umuhimu wa kupunguza matumizi ya damu.”
Wenye Mamlaka Nchini Urusi Wajaribu Kunyakua Mali Inayomilikiwa na Shirika la Mashahidi wa Yehova la Marekani
Mahakama ya Jiji la Saint Petersburg itasikiliza rufaa ya Mashahidi wa Yehova kuhusu hukumu iliyotolewa ya kunyakua ofisi yao ya kitaifa nchini Urusi.
Makusanyiko ya Kila Mwaka ya Mashahidi wa Yehova ya 2018 Yataanza Mwezi wa Mei
Kabla ya tukio hilo kuanza, Mashahidi ulimwenguni pote watashiriki katika kampeni ya ulimwenguni pote ya kuwakaribisha watu wote kuhudhuria programu hiyo bila malipo.