Kiswahili
Hakimu Kutoa Uamuzi Katika Kesi ya Mashahidi 16 wa Yehova Jijini Taganrog
/assets/ct/79e1b14fff/images/syn_placeholder_sqr.png

NOVEMBA 20, 2015
URUSI

Hakimu Kutoa Uamuzi Katika Kesi ya Mashahidi 16 wa Yehova Jijini Taganrog

Hakimu Kutoa Uamuzi Katika Kesi ya Mashahidi 16 wa Yehova Jijini Taganrog

Hakimu Vasyutchenko wa Mahakama ya Jiji la Taganrog ametangaza kuwa atatoa uamuzi wa kesi ya Mashahidi 16 wa Yehova Novemba 27, 2015, saa 4:30 asubuhi, kwa Saa za Moscow. Watuhumiwa wameshtakiwa kwa kujihusisha na shughuli zenye msimamo mkali kwa kupanga na kuhudhuria mikutano ya dini, ambapo wanazungumzia Biblia kwa amani. Ikiwa watapatikana kuwa na makosa, wote watalazimika kulipa faini kubwa, na wanne kati yao huenda wakafungwa gerezani kwa miaka sita.

Anwani ya mahakama ni 347939, g. Taganrog, ul. Chucheva, d. 42/2.