Kiswahili
Mahakama Kuu ya Urusi Yatoa Uamuzi Dhidi ya Mashahidi wa Yehova
https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/702017119/univ/art/702017119_univ_sqr_xl.jpg

APRILI 20, 2017
URUSI

Mahakama Kuu ya Urusi Yatoa Uamuzi Dhidi ya Mashahidi wa Yehova

Mahakama Kuu ya Urusi Yatoa Uamuzi Dhidi ya Mashahidi wa Yehova

NEW YORK—Baada ya kusikiliza kesi kwa siku sita katika majuma mawili yaliyopita, Mahakama Kuu ya Shirikisho la Urusi leo imeunga mkono dai lililowasilishwa na Wizara ya Haki la kufunga Kituo cha Usimamizi cha Mashahidi wa Yehova nchini Urusi pamoja na mashirika 395 ya kidini (Local Religious Organizations au LRO) yanayotumiwa na Mashahidi kotekote nchini Urusi. Uamuzi huo unaanza kutumika mara moja.

Yaroslav Sivulskiy, msemaji wa Mashahidi wa Yehova nchini Urusi anasema hivi: “Tunasikitishwa sana na uamuzi huo na tuna wasiwasi mwingi jinsi utakavyoathiri utendaji wetu wa kidini. Tutakata rufaa, na tunatumaini kwamba tutarudishiwa upesi haki zetu za kisheria na ulinzi tunaopaswa kupewa tukiwa kikundi cha kidini kilicho na amani.”

Mashahidi wa Yehova nchini Urusi wana siku 30 za kuwasilisha rufaa yao ili ikaguliwe na jopo la watu watatu.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000

Urusi: Yaroslav Sivulskiy, +7-911-087-8009