Kiswahili
Ndugu Makhalichev Aachiliwa Kutoka Gerezani Nchini Belarus, Mwendesha Mashtaka Akataa Ombi la Kumrudisha Urusi
https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/702020214/univ/art/702020214_univ_sqr_xl.jpg

Ndugu Nikolay Makhalichev baada ya kuachiliwa huru nchini Belarus

APRILI 9, 2020
URUSI

Ndugu Makhalichev Aachiliwa Kutoka Gerezani Nchini Belarus, Mwendesha Mashtaka Akataa Ombi la Kumrudisha Urusi

Ndugu Makhalichev Aachiliwa Kutoka Gerezani Nchini Belarus, Mwendesha Mashtaka Akataa Ombi la Kumrudisha Urusi

Aprili 7, 2020, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka nchini Belarus ilikataa kutenda kulingana na ombi la Urusi la kumsafirisha Ndugu Nikolay Makhalichevna hivyo kumweka huru. Ndugu Nikolay Makhalichev alifurahi sana kwa kuwa alipata nafasi ya kuhudhuria Ukumbusho wa Kifo cha Yesu akiwa huko Belarus pamoja rafiki zake.

Februari 21, 2020, wenye mamlaka walimkamata Ndugu Nikolay Makhalichev alipokuwa akisafiri kutoka Urusi kuelekea Belarus ili kuwatembelea rafiki zake. Polisi wa Belarus walipoona pasipoti yake waliamua kumweka chini ya ulinzi huku wakifanya uchunguzi, baadaye waligundua kwamba alikuwa katika orodha ya watu wanaotafutwa nchini Urusi kwa kosa la kupanga “shughuli zenye msimamo mkali.”

Baada ya siku tatu, wakaamua kumkamata Ndugu Nikolay Makhalichev, ingawa hawakuwa wameamua ikiwa wangemrudisha Urusi kwa ajili ya kesi yake iliyofunguliwa Januari 2019. Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Shahidi wa Yehova kukamatwa katika nchi nyingine kwa mamlaka iliyotolewa na hakimu nchini Urusi.

Ndugu Nikolay Makhalichev aliendelea kuwa na mtazamo mzuri alipokuwaamekamatwa kwa kudumisha ratiba nzuri ya kiroho. Hata aliongoza mafunzo manne ya Biblia na kuripoti saa 198 za huduma katika mwezi wa Machi.

Tuna uhakika kwamba ndugu na dada zetu nchini Urusi wataendelea kumtegemea Yehova awasaidie na kuwalinda kwa kuwa yeye ni kimbilio lao wakati wa taabu.—Zaburi 142:5.