Kiswahili
Kuendelea Kuwa Washikamanifu na Wenye Shangwe kwa Msaada wa Yehova
https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/702025005/univ/art/702025005_univ_sqr_xl.jpg

OKTOBA 13, 2025
URUSI

Kuanzia kushoto hadi kulia, safu ya kwanza: Vasiliy Bondarev, Ivan Nikitin, Nikolay Kovadnev, na Radion Shitov. Safu ya katikati: Sergey Sachnev, Svetlana Zharkova, Marina Voytko, na Mikhail Dorofeyev. Safu ya mwisho: Ulita Sachneva na Irina Bondareva

Kuendelea Kuwa Washikamanifu na Wenye Shangwe kwa Msaada wa Yehova

Kuendelea Kuwa Washikamanifu na Wenye Shangwe kwa Msaada wa Yehova

Oktoba 1, 2025, Mahakama ya Wilaya ya Komsomolskiy iliyo katika Eneo la Khabarovsk iliwahukumu Vasiliy Bondarev, Irina Bondareva, Mikhail Dorofeyev, Nikolay Kovadnev, Ivan Nikitin, Sergey Sachnev, Ulita Sachneva, Radion Shitov, Marina Voytko, na Svetlana Zharkova. Mikhail, Nikolay, na Radion walihukumiwa kifungo cha nje cha miaka sita kila mmoja. Vasiliy, Irina, Ivan, Sergey, Ulita, Marina, na Svetlana walihukumiwa kifungo cha nje cha miaka miwili kila mmoja. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunapoendelea kuvumilia changamoto za siku hizi za mwisho, tunawakumbuka ndugu na dada zetu wanaoteswa na tunashangilia pamoja nao wanapoendelea kumpa Yehova utukufu kupitia imani yao.​—1 Wakorintho 12:25, 26.