Hamia kwenye habari

Kushoto kwenda kulia: Ndugu Oleg Konshin, Ndugu Sergey Malyanov, na Dada Svetlana Malyanova

NOVEMBA 28, 2022 | HABARI ZILIONGEZWA: APRILI 27, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—WATOZWA FAINI | Kumtegemea Yehova Kumeondoa Wasiwasi

HABARI ZA KARIBUNI—WATOZWA FAINI | Kumtegemea Yehova Kumeondoa Wasiwasi

Aprili 26, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Leninskiy iliyo Nizhny Novgorod iliwahukumu Ndugu Oleg Konshin, Ndugu Sergey Malyanov, Ndugu Roman Zhivolupov a na Dada Svetlana Malyanova, ambaye ni binti ya Sergey. Mahakama iliwatoza faini ya kuanzia rubo 450,000 (dola 5,494 za Marekani) hadi rubo 700,000 (dola 8,546 za Marekani).

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Ndugu na dada zetu wanaoendelea kuwa waaminifu licha ya mateso wanayokabili ni ushahidi hakika wa kwamba wale ‘wanaomtumaini Yehova watakuwa jasiri na wenye moyo mkuu.’​—Zaburi 27:14.

Mfuatano wa Matukio

  1. Februari 7, 2019

    Hakimu alimruhusu ofisa wa polisi kufuatilia simu ambazo Sergey anapiga na kupokea na hata njia nyingine za mawasiliano ya kielektroni anazotumia

  2. Julai 16-17, 2019

    Maofisa wa polisi walifanya msako katika nyumba 31 za Mashahidi wa Yehova wanaoishi katika Eneo la Nizhny Novgorod. Oleg, Sergey, na Svetlana walikamatwa na kupelekwa kizuizini. Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi yao

  3. Julai 18, 2019

    Oleg, Sergey, na Svetlana waliruhusiwa kutoka kizuizini. Mahakama iliwazuia ndugu hao wawili kuwasiliana wao kwa wao, kuondoka nyumbani muda fulani, au kutumia Intaneti

  4. Agosti 24, 2021

    Roman alishtakiwa rasmi kwa sababu ya kushiriki katika utendaji wa shirika lenye msimamo mkali na akawekewa vizuizi vya kusafiri

  5. Machi 3, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza

a b Picha ya Ndugu Roman Zhivolupov haikupatikana makala hii ilipokuwa ikitayarishwa.