Kiswahili
HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAFUNGWA BAADA YA RUFAA | Tunathamini Sana Pendeleo la Kumtumikia Yehova
https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/702024081/univ/art/702024081_univ_sqr_xl.jpg

Kushoto: Ndugu Yevgeniy Stefanidin. Kulia: Ndugu Aleksandr Votyakov

APRILI 23, 2024 | HABARI ZIMEONGEZWA: FEBRUARI 7, 2024
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAFUNGWA BAADA YA RUFAA | Tunathamini Sana Pendeleo la Kumtumikia Yehova

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAFUNGWA BAADA YA RUFAA | Tunathamini Sana Pendeleo la Kumtumikia Yehova

Februari 4, 2025, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Udmurtian ilibadili vifungo vya nje vya Ndugu Yevgeniy Stefanidin na Ndugu Aleksandr Votyakov baada ya kesi ya rufaa. Ndugu Yevgeniy Stefanidin sasa atatumikia kifungo cha miaka sita gerezani, na Ndugu Aleksandr Votyakov atatumikia kifungo cha miaka sita na miezi sita gerezani. Walipelekwa gerezani moja kwa moja baada ya kutoka mahakamani.

Oktoba 25, 2024 Mahakama ya Pervomayskiy iliyo katika Wilaya ya Izhevsk katika Jamhuri ya Udmurtian, iliwahukumu Ndugu Yevgeniy Stefanidin na Ndugu Aleksandr Votyakov. Ndugu Yevgeniy alihukumiwa kifungo cha nyumbani cha miaka sita na Ndugu Aleksandr kifungo cha nyumbani cha miaka sita na nusu. Hawahitaji kwenda gerezani kwa sasa.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Kama Aleksandr na Yevgeniy, tunaliona kuwa pendeleo kubwa “Kumtolea [Yehova] utumishi mtakatifu bila woga” siku zetu zote.​—Luka 1:74, 75.

Mfuatano wa Matukio

  1. Aprili 14, 2021

    Maofisa wa usalama walifanya msako kwenye nyumba ya Yevgeniy

  2. Desemba 13, 2022

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Aleksandr na Yevgeniy

  3. Desemba 14, 2022

    Maofisa walifanya msako kwenye nyumba ya Aleksandr na ya Yevgeniy. Aleksandr alipelekwa mahabusu. Yevgeniy aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  4. Desemba 15, 2022

    Aleksandr aliachiliwa kutoka mahabusu na akawekwa katika kifungo cha nyumbani

  5. Juni 9, 2023

    Aleksandr aliachiliwa kutoka katika kifungo cha nyumbani na akawekewa vizuizi vya kusafiri

  6. Agosti 17, 2023

    Kesi ya uhalifu ilianza