Kiswahili
HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU NA DADA WAFUNGWA | Imani Katika Yehova Hutusaidia Kushinda Woga Tunapoteswa
https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/702022166/univ/art/702022166_univ_sqr_xl.jpg

Kushoto: Dada Marina Chaplykina. Kulia: Ndugu Valeriy Maletskov na mke wake, Marina

AGOSTI 18, 2022 | HABARI ZA KARIBUNI: DESEMBA 19, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU NA DADA WAFUNGWA | Imani Katika Yehova Hutusaidia Kushinda Woga Tunapoteswa

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU NA DADA WAFUNGWA | Imani Katika Yehova Hutusaidia Kushinda Woga Tunapoteswa

Desemba 18, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Novosibirsk iliyo katika Eneo la Novosibirsk ilimhukumu Ndugu Valeriy Maletskov kifungo cha miaka sita gerezani. Dada Marina Chaplykina alihukumiwa miaka minne gerezani. Wote walipelekwa kizuizini moja kwa moja kutoka mahakamani.

Mfuatano wa Matukio

  1. 2018

    Mwanamume aliyekuwa anajifunza Biblia na kuhudhuria mikutano ya Mashahidi wa Yehova kabla hajakamatwa, alianza kushirikiana na wapelelezi wa FSB katika eneo la Novosibirsk, na kutoa taarifa za wale waliokuwa wakihudhuria mikutano.

  2. Aprili 19, 2019

    Kupitia taarifa zilizotolewa na mwanamume huyo, nyumba sita za Mashahidi wa Yehova katika eneo la Novosibirsk zilifanyiwa msako. Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Valeriy Maletskov na Marina Chaplykina. Wote wawili walipelekwa mahabusu baada ya kukamatwa.

  3. Aprili 21, 2019

    Wote wawili waliachiliwa kutoka mahabusu. Valeriy aliwekwa katika kifungo cha nyumbani, na Marina Chaplykina aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  4. Februari 21, 2022

    Valeriy alishtakiwa kwa kuendesha shughuli za shirika lenye msimamo mkali. Marina Chaplykina alishtakiwa kwa kutegemeza kifedha utendaji wa shirika lenye msimamo mkali

  5. Machi 30, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Ujasiri na uvumilivu wa wale wanaokabili mateso kwa sababu ya imani yao ni uthibitisho wa baraka na ulinzi wa Yehova.