DESEMBA 16, 2022 | HABARI ZIMEONGEZWA: JUNI 20, 2023
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AFUNGWA | Ana Shangwe Licha ya Magumu Yanayoendelea
Juni 20, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Tsentralnyi iliyoko Sochi ilimhukumu Ndugu Danil Suvorov kifungo cha miaka sita gerezani. Danil amekuwa kizuizini tangu Agosti 18, 2021, na ataendelea kubaki humo.
Maelezo Mafupi Kumhusu
Tunafarijiwa tunapojua kwamba tukiendelea kufanya mambo ya kiroho kwa bidii na kudumisha urafiki wa karibu na Yehova, tutaendelea kuwa na shangwe, licha ya changamoto zozote ambazo huenda tukakabili.—Zaburi 16:11.
Mfuatano wa Matukio
Agosti 13, 2021
Kesi ya uhalifu ilianzishwa kwa kutegemea ushahidi wa mtu ambaye alikuwa akishirikiana na wenye mamlaka huku akijifanya kwamba angependa kujua mengi zaidi kuhusu Biblia
Agosti 18, 2021
Msako ulifanywa nyumbani kwao. Alikamatwa na kuwekwa kizuizini
Agosti 19, 2021
Alihamishwa na kupelekwa mahabusu
Aprili 29, 2022
Alishtakiwa rasmi kwa kupanga, kushiriki, na kuwashawishi wengine kujiunga na utendaji wa shirika lenye msimamo mkali
Juni 10, 2022
Kesi ya uhalifu ilianza

