Kiswahili
HABARI ZA KARIBUNI—DADA WAHUKUMIWA | Kukabiliana na Majaribu Huku Wakimtumaini Yehova
https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/702024071/univ/art/702024071_univ_sqr_xl.jpg

Kushoto kwenda kulia: Dada Yekaterina Olshevskaya, Dada Kristina Golik, Dada Valentina Yermilova, na Dada Mariya Myasnikova

FEBRUARI 9, 2024 | HABARI ZIMEONGEZWA: DESEMBA 6, 2024
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—DADA WAHUKUMIWA | Kukabiliana na Majaribu Huku Wakimtumaini Yehova

HABARI ZA KARIBUNI—DADA WAHUKUMIWA | Kukabiliana na Majaribu Huku Wakimtumaini Yehova

Desemba 6, 2024, Mahakama ya Jiji la Blagoveshchensk iliyo katika Eneo la Amur iliwahukumu Dada Kristina Golik, Dada Yekaterina Olshevskaya, Dada Mariya Myasnikova, na Dada Valentina Yermilova. Kristina na Valentina walihukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka miwili na miezi sita na watafanya kazi ya kulazimishwa. Mariya na Yekaterina walihukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka miwili na miezi miwili na watafanya kazi ya kulazimishwa. Wote wanne watakaa gerezani na watakuwa wakienda kufanya kazi walizopangiwa katika jamii.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunamshukuru Yehova kwa vielelezo ambavyo dada hawa wanatuwekea. Na tunajua kwamba Yehova ataendelea kuwatunza na kuwabariki.​—Zaburi 27:3.

Mfuatano wa Matukio

  1. Julai 20, 2018

    Nyumba zilifanyiwa msako

  2. Julai 22, 2021

    Dada wote wanne walishtakiwa kuwa wahalifu

  3. Julai 27, 2021

    Kristina na Mariya waliwekewa vizuizi vya kusafiri

  4. Agosti 3, 2021

    Yekaterina aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  5. Agosti 4, 2021

    Valentina aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  6. Mei 26, 2023

    Kesi ya uhalifu ilianza