SEPTEMBA 7, 2023
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE
Kimbunga Idalia Chapiga Magharibi mwa Kuba na Kusini Mashariki mwa Marekani
Agosti 29, 2023, Dhoruba ya Kitropiki Idalia ilipiga mkoa wa Pinar del Río ulio magharibi mwa Kuba na kusababisha upepo mkali na mvua nyingi. Dhoruba hiyo iliongezeka ikawa kimbunga kikubwa chenye upepo uliovuma kwa kasi ya zaidi ya kilometa 200 kwa saa. Agosti 30, 2023, Kimbunga Idalia kilifika kwenye ufuo wa Keaton ulio kwenye pwani ya Florida, Marekani inayopakana na Ghuba ya Mexico. Baadaye, kimbunga hicho kilipungua kikawa tena dhoruba ya kitropiki. Dhoruba hiyo ilisababisha upepo mkali, mvua kubwa, na mafuriko katika maeneo ya Florida, Georgia, North Carolina, na South Carolina. Isitoshe, umeme pia ulikatika katika maeneo hayo.
Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata
Kuba
Hakuna ndugu au dada yetu ambaye alikufa
Mhubiri 1 alilazimika kuhama makao yake
Nyumba 1 iliharibiwa kabisa
Nyumba 12 zilipata uharibifu mdogo
Marekani
Hakuna ndugu au dada yetu ambaye alikufa
Mhubiri 1 alijeruhiwa kidogo
Wahubiri 1,297 walilazimika kuhama makao yao
Nyumba 4 ziliharibiwa kabisa
Nyumba 12 zilipata uharibifu mkubwa
Nyumba 61 zilipata uharibifu mdogo
Jumba 1 la Ufalme lilipata uharibifu mkubwa
Majumba 3 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo
Jitihada za Kutoa Msaada
Nchini Kuba na nchini Marekani wazee na waangalizi wa mzunguko wa maeneo yaliyoathiriwa wanaandaa msaada wa kiroho na wa kimwili kwa ajili ya akina ndugu na dada
Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kuwategemeza wote walioathiriwa na Kimbunga Idalia.—Isaya 63:9.

