MACHI 31, 2025 | HABARI ZIMEONGEZWA: APRILI 24, 2025
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE
Majengo yakiwa yameanguka nchini Myanmar (kushoto) na Thailand (kulia) baada ya tetemeko la ardhi lililotokea Machi 28, 2025
HABARI ZA KARIBUNI—Tetemeko Kubwa la Ardhi Latikisa Myanmar na Thailand
Machi 28, 2025, tetemeko kubwa la ardhi lenye kipimo cha 7.7 liliipiga Myanmar. Tetemeko hilo na matetemeko mengine madogo yaliyotokea baadaye yalisababisha uharibifu mkubwa wa madaraja, majengo, na barabara kotekote katika jiji la Mandalay. Ripoti kutoka katika nchi hiyo zinaonyesha kwamba zaidi ya watu 3,400 walijeruhiwa, wengine 300 hivi hawajulikani waliko na zaidi ya watu 1,700 walikufa.
Isitoshe, tetemeko hilo kubwa la ardhi lilifika jijini Bangkok, Thailand, umbali wa kilomita 1,300 hivi kutoka Myanmar, na kusababisha jengo refu la ghorofa kuanguka. Watu 18 walikufa nchini Thailand, 33 wakajeruhiwa, na zaidi ya 75 bado hawajulikani waliko.
Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata
Myanmar
Kwa kusikitisha kuna mume na mke waliokufa
Wahubiri 9 walijeruhiwa
Wahubiri 142 walilazimika kuhama makazi yao
Nyumba 6 ziliharibiwa kabisa
Nyumba 25 zilipata uharibifu mkubwa
Nyumba 52 zilipata uharibifu mdogo
Majumba 2 ya Ufalme yalipata uharibifu mkubwa
Majumba 4 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo
Thailand
Hakuna ndugu au dada yetu aliyekufa kutokana na tetemeko hilo
Wahubiri 2 wamejeruhiwa
Wahubiri 52 wamelazimika kuhama makazi yao
Nyumba 4 zilipata uharibifu mkubwa
Nyumba 69 zilipata uharibifu mdogo
Majumba 8 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo
Jitihada za Kutoa Msaada
Waangalizi wa mzunguko na wazee wa maeneo hayo wanatoa msaada wa kiroho na wa kimwili kwa walioathiriwa
Halmashauri 1 ya Kutoa Msaada imewekwa rasmi nchini Myanmar ili kusimamia kazi ya kutoa msaada
Tunasikitishwa na vifo na uharibifu uliosababishwa na tetemeko hilo la ardhi. Tukiwa na imani yenye nguvu katika ahadi za Mungu, tunatazamia wakati ujao ambapo “sauti ya kulia na ya maombolezo kwa sababu ya taabu haitasikika tena.”—Isaya 65:19.

