Kiswahili
Ndugu Artur Yangibayev Afungwa Gerezani kwa Mara ya Pili kwa Kukataa Kujiunga na Jeshi kwa Sababu ya Dhamiri
https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/702021002/univ/wpub/702021002_univ_sqr_xl.jpg

FEBRUARI 8, 2021
TURKMENISTAN

Ndugu Artur Yangibayev Afungwa Gerezani kwa Mara ya Pili kwa Kukataa Kujiunga na Jeshi kwa Sababu ya Dhamiri

Ndugu Artur Yangibayev Afungwa Gerezani kwa Mara ya Pili kwa Kukataa Kujiunga na Jeshi kwa Sababu ya Dhamiri

Hukumu

Januari 18, 2021, mahakama nchini Turkmenistan ilimhukumu Ndugu Artur Yangibayev kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri. Hii ndiyo mara ya pili kuhukumiwa kuwa na hatia kwa sababu ya msimamo wake wa kutounga mkono upande wowote.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Artur Yangibayev

  • Alizaliwa: 1997 (Seydi)

  • Maisha Yake: Artur alikabili changamoto alipokuwa mtoto, ambazo zilimfanya ajiulize kwa nini kuna ukosefu mwingi wa haki ulimwenguni. Alizungumzia jambo hilo pamoja na dada yake, ambaye ni Shahidi wa Yehova. Hivyo akaanza kujifunza Biblia akiwa na umri wa miaka 13. Alibatizwa mwaka wa 2014

    Anafanya kazi ya ujenzi, akirekebisha majengo ya makazi. Wazazi wa Artur wanasema yeye ni mwana mwenye fadhili na mwenye kuwajibika. Majirani wanamheshimu kwa sababu ni kijana mnyoofu katika jamii yao

Historia ya Kesi

Agosti 8, 2016, Artur aliwekwa mahabusu kwa kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri. Agosti 30 alihukumiwa kifungo cha miaka miwili ya kazi ya kurekebisha tabia. Mnamo Septemba 2018, Artur alimaliza muda wa hukumu hiyo ya kazi ya kurekebisha tabia.

Desemba 15, 2020, aliitwa jeshini kwa mara ya pili. Punde baada ya hapo alihojiwa na mwendesha-mashtaka na kuambiwa aandike sababu zake za kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri.

Desemba 30, ofisi ya mwendesha-mashtaka ilimjulisha kwamba wamefungua kesi ya uhalifu dhidi yake. Wenye mamlaka walimnyang’anya pasipoti yake.

Artur anasema kwamba baada ya kumaliza kifungo chake cha kwanza “mistari ya Biblia kwenye Waroma 8:37-39 ilinipa uhakika wa kwamba hakuna anayeweza kunizuia kuendelea kuwa mwaminifu kwa Yehova.” Tunajua kwamba kwa msaada wa Yehova, Artur ataweza kuvumilia jaribu hili pia.