Kiswahili
Mahakama ya Kijeshi ya Turkmenstan Yamhukumu Ndugu Ruslan Artykmyradov Miaka Miwili Gerezani
/assets/ct/79e1b14fff/images/syn_placeholder_sqr.png

JANUARI 13, 2021
TURKMENISTAN

Mahakama ya Kijeshi ya Turkmenstan Yamhukumu Ndugu Ruslan Artykmyradov Miaka Miwili Gerezani

Mahakama ya Kijeshi ya Turkmenstan Yamhukumu Ndugu Ruslan Artykmyradov Miaka Miwili Gerezani

Januari 11, 2021, Mahakama ya kijeshi ya Turkmenstan ilimhukumu Ndugu Ruslan Artykmyradov kifungo cha miaka miwili gerezani. Hii ni mara yake ya pili kufungwa gerezani kwa sababu ya kutounga mkono upande wowote.

Baada ya hukumu kutangazwa Ruslan hakuwa amevunjika moyo, badala yake alitabasamu. Alipokuwa akipelekwa gerezani, alinukuu maneno ya Yesu katika Mathayo 24:13: “Yule atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa.”

Tunatiwa moyo na imani ya ndugu zetu vijana nchini Turkmenistan. Wanafuata kwa hiari Kielelezo chetu, Yesu, aliyevumilia mengi “kwa sababu ya shangwe iliyowekwa mbele yake.”—Waebrania 12:2.