JUNI 20, 2019
MEXICO
Monterrey, Mexico—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”!
Tarehe: Juni 7-9, 2019
Mahali: Uwanja wa Michezo wa BBVA Bancomer wa Monterrey, Mexico
Lugha ya Programu: Kiingereza, Lugha ya Ishara ya Mexico, Kihispania
Maeneo Yaliyounganishwa: 38 katika nchi 6 (Kosta Rika, Guatemala, Honduras, Mexico, Nikaragua, na Panama)
Idadi ya Wahudhuriaji: 39,099
Idadi ya Waliobatizwa: 393
Idadi wa Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 4,682
Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Argentina, Brazili, Kolombia, Ufaransa, Italia, Japani, Uholanzi, Paraguai, Peru, Hispania, Marekani
Mambo Yaliyoonwa: Roberto Valero, mwakilishi wa meya katika jiji la Guadalupe, alitembelea eneo la kusanyiko siku ya Jumamosi. Kati ya mambo mengine, alisema hivi: “Serikali imeazimia kudumisha amani na usalama wa watu wake. Na ninyi Mashahidi wa Yehova, mmechangia sana kwa kuwa raia wema. Jiji zima linatambua hilo.”
Ndugu na dada wakiwakaribisha wajumbe katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Monterrey
Wajumbe wakifika kusanyikoni, Mlima Silla unaovutia unaonekana upande wa nyuma
Ndugu Mark Sanderson, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akitoa hotuba ya mwisho siku ya Ijumaa
Mtu akibatizwa Jumamosi katika moja ya vidimbwi vinne vilivyotumiwa kusanyikoni
Wajumbe wa mataifa mbalimbali wakisikiliza kwa makini programu ya kusanyiko
Watumishi wa pekee wa wakati wote wakiwapungia watu mkono siku ya mwisho ya kusanyiko
Familia kutoka Apodaca, Mexico, wakiwa wameshika bango linalosema, ‘Tunawapenda’
Mjumbe na dada mwenyeji wakihubiri katika eneo la Monterrey
Wajumbe wafurahia dansi kutoka Mexico kaskazini inayoitwa Polka Norteña
Dada wakicheza dansi ya kitamaduni ya jimbo la Jalisco, Mexico

