Kiswahili
Mashahidi wa Yehova Wamaliza Kuuza Maeneo Yote ya Brooklyn, One York Street
/assets/ct/28ada02fb0/images/syn_placeholder_sqr.png

DESEMBA 13, 2018
MAREKANI

Mashahidi wa Yehova Wamaliza Kuuza Maeneo Yote ya Brooklyn, One York Street

Mashahidi wa Yehova Wamaliza Kuuza Maeneo Yote ya Brooklyn, One York Street

Desemba 12, 2018, Mashahidi wa Yehova waliuza eneo la mwisho kati ya maeneo ya makao makuu ya Brooklyn, Mtaa wa One York, ambao pia unajulikana kuwa Mtaa wa 30 Front, wamewauzia shirika la Fortis Dumbo Acquisition, LLC. Tangu mwaka wa 2004, Mashahidi wameuza maeneo 37 waliyomiliki Brooklyn.

Baada ya kununua eneo la York Street mwaka wa 1977, Mashahidi walilitumia kuegesha magari ya wale waliofanya kazi katika makao makuu ya zamani. Sehemu iliyoonyeshwa kwenye picha ipo katika eneo la kihistoria la DUMBO na mpaka wake unafika chini ya Daraja la Brooklyn hadi Brooklyn-Queens Expressway.

Kwa miaka zaidi ya 100, Mashahidi wameelekeza kazi yao ya elimu ya Biblia kutoka makao makuu yaliyokuwa Brooklyn. Tangu mwaka wa 2016, Mashahidi wamesimamia kazi yao ya ulimwenguni pote kutoka makao makuu mapya yaliyoko Warwick, New York.

Wanahabari wanaweza kuwasiliana na: Ofisi ya Habari za Umma, +1-845-524-3000