APRILI 16, 2019
MAREKANI
Mafuriko Makubwa Yakumba Magharibi ya Marekani
Mvua kubwa na barafu iliyoyeyuka ilisababisha mafuriko katika maeneo ya Nebraska na Iowa katikati ya mwezi wa Machi 2019. Kiwango cha maji katika mito kiliongezeka kuliko wakati mwingine wowote, maji hayo yalipasua mabwawa na mabomba ya kuzuia maji, na kuharibu nyumba nyingi sana, na hata kuua watu wanne hivi.
Ofisi ya tawi ya Marekani imeripoti kwamba hakuna yeyote kati ya wahubiri 5,123 wanaoishi katika eneo hilo aliyepoteza maisha au kupata majeraha. Hata hivyo, wahubiri 84 wamelazimika kuhama. Nyumba 8 za akina ndugu zimeharibiwa kabisa na nyingine 34 zimeharibiwa kwa kiwango fulani.
Wajitoleaji katika makutaniko yaliyo karibu wameanza kushiriki katika usafi, kwa msaada wa kikosi cha Usanifu-Majengo na Ujenzi. Waangalizi wa mzunguko katika maeneo yaliyoathiriwa na janga hilo wamefanya mipango ili walioathiriwa wapate ziara za uchungaji.
Tunasali kwamba ndugu zetu waendelee kupata faraja kutokana na msaada wa kimwili na wa kiroho wanaopata wakati wa majaribu haya.—2 Wakorintho 1:3, 4.

