Matukio Muhimu Kihistoria Nchini Korea Kusini
OKTOBA 18, 2016—Kwa mara ya kwanza Mahakama ya Rufaa ya Gwangju yatoa uamuzi kwamba watu watatu waliokataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri hawakuwa wamefanya kosa
JANUARI 14, 2015—CCPR yatoa uamuzi na kutangaza kwamba Korea Kusini ilikiuka haki za watu 50 waliokataa utumishi wa kijeshi kwa kuwapa “vifungo visivyo vya haki”
SOMA ZAIDI
OKTOBA 25, 2012—Katika kesi ya Mashahidi 388, CCPR yatoa uamuzi wa kwamba haki yao ya kuwa na uhuru wa dhamiri haikuheshimiwa
AGOSTI 30, 2011—Mahakama ya Kikatiba yatoa tena uamuzi wa kuadhibu wale wanaokataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri
MACHI 24, 2011—CCPR yachunguza hati za Mashahidi 100 na kutoa uamuzi kwamba mtu ana haki ya kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri
MACHI 23, 2010—CCPR yatangaza kwamba haki za watu 11 ambao si Mashahidi zilikiukwa kwa sababu haki yao ya kuwa na uhuru wa dhamiri haikuheshimiwa walipokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri
JANUARI 15, 2009—Ripoti ya rais yaonyesha kwamba serikali inawajibika kwa vifo vya Mashahidi watano waliofungwa gerezani kwa kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri kati ya mwaka 1975 hadi 1985
NOVEMBA 3, 2006—Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu yatangaza Korea Kusini ilikiuka haki za Mashahidi wawili waliokataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri
AGOSTI 26, 2004—Mahakama ya Kikatiba yaunga mkono sheria ya kuwaadhibu wale wanaokataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri
1975—Serikali yaanzisha mpango wa kuandikisha watu jeshini kwa lazima
1973—Serikali yaanza kuwatesa Mashahidi waliofungwa gerezani na yaendelea kufanya hivyo hadi mwaka wa 1995 hivi
1953—Serikali ilimfunga gerezani Shahidi wa kwanza aliyekataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri
OKTOBA 30, 1952—Serikali yasajili The Watch Tower Songso Chaekja Hyuphoi of Korea

