OKTOBA 6, 2025
FILIPINO
Nyumba ya dada huko Gahit, Cataingan, katika jiji la Masbate, baada ya kuharibiwa na upepo mkali uliosababishwa na Kimbunga Bualoi
Kimbunga Bualoi Chasababisha Uharibifu Mkubwa Nchini Filipino
Septemba 25, 2025, Kimbunga Bualoi a kilifika kwenye nchi kavu katika Jimbo la Samar Mashariki nchini Filipino. Kimbunga hicho kiliambatana na mvua kubwa na upepo uliokuwa ukivuma kwa kasi ya kilomita 165 kwa saa. Hali hizo zilisababisha mafuriko, maporomoko ya ardhi, na uharibifu mkubwa wa nyumba na barabara katika maeneo mengi ambayo kimbunga hicho kilipita. Wenye mamlaka wanakadiria kwamba watu milioni 2.1 hivi waliathiriwa. Kwa kusikitisha, watu 13 walikufa nchini Filipino.
Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata
Hakuna ndugu au dada yetu aliyekufa au kujeruhiwa
Wahubiri 142 walilazimika kuhama makazi yao
Nyumba 53 ziliharibiwa kabisa
Nyumba 104 zilipata uharibifu mkubwa
Nyumba 187 zilipata uharibifu mdogo
Jumba 1 la Ufalme lilipata uharibifu mkubwa
Majumba 7 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo
Jitihada za Kutoa Msaada
Waangalizi wa mzunguko na wazee wa eneo hilo, wanaendelea kushughulikia mahitaji ya kiroho na ya kimwili ya walioathiriwa na kimbunga hicho
Halmashauri 3 za Kutoa Msaada zinasimamia jitihada za kutoa msaada
Katika kipindi hiki kigumu, tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kuwaimarisha ndugu na dada zetu ambao wameathiriwa na kimbunga hicho nchini Filipino.—Wafilipi 4:13.
a Kimbunga hiki kinaitwa Opong, nchini Filipino.

