Kiswahili
Mafuriko Makubwa na Maporomoko ya Ardhi Yatokea Kusini mwa Japani
https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/702025143/univ/art/702025143_univ_sqr_xl.jpg

AGOSTI 25, 2025
JAPANI

Nguzo ya umeme imelalia nyumba ambayo ilianguka baada ya maporomoko ya ardhi katika mji wa Misato, Eneo la Kumamoto, Japani

Mafuriko Makubwa na Maporomoko ya Ardhi Yatokea Kusini mwa Japani

Mafuriko Makubwa na Maporomoko ya Ardhi Yatokea Kusini mwa Japani

Kuanzia Agosti 8, 2025, mvua kubwa zilinyesha kwenye kisiwa cha Kyushu kilicho kusini mwa Japani, kwa siku nne. Katika mji mmoja, mvua yenye kipimo cha sentimita 37 ilinyesha ndani ya saa sita. Zaidi ya mafuriko, baadhi ya maeneo yalikuwa pia na maporomoko ya ardhi ambayo yaliharibu kabisa nyumba za watu, barabara, na mashamba. Kwa sababu ya hatari iliyokuwepo, wenye mamlaka waliagiza watu waondoke kwenye eneo hilo. Mamilioni ya watu walilazimika kuondoka. Watu nane hivi walikufa.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Kwa kusikitisha, dada mwenye umri wa miaka 71 pamoja na mume wake walikufa

  • Mhubiri 1 alijeruhiwa

  • Wahubiri 22 walilazimika kuhama makazi yao

  • Nyumba 13 zilipata uharibifu mkubwa

  • Nyumba 87 zilipata uharibifu mdogo

  • Jumba 1 la Ufalme lilipata uharibifu mdogo

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Waangalizi wa mzunguko na wazee wa maeneo hayo wanaendelea kushughulikia mahitaji ya kiroho na ya kimwili ya walioathiriwa

Tunasikitishwa sana na vifo vilivyosababishwa na janga hili. Hata hivyo, tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kuwapa “uvumilivu na faraja” wote walioathiriwa na janga hili.​—Waroma 15:5.